Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali jinai ya kutisha iliyofanywa na kundi la kigaidi la Harakati la Nureddin al-Zenki ya kumchinja mtoto wa Kipalestina.
Taarifa iliyotolewa na Hizbullah imelaani vikali jinai hiyo ya kutisha iliyofanywa na kundi la kigaidi la Harakati la Nureddin al-Zenki inayosaidiwa na Marekani na waitifaki wake ya kumkata kichwa mateka huyo mtoto wa Kipalestina katika kambi ya wakimbizi ya Handarat huko kaskazini mwa Halab (Aleppo) nchini Syria na kisha kuonesha kichwa cha mtoto huyo mbele ya umati wa watu.
Taarifa ya Hizbullah imesema kuwa, jinai hiyo ya kuchukiza ni sehemu ya vita vya pande zote dhidi ya taifa linalodhulumiwa la Palestina.
Imesema hatua ya baadhi ya nchi kulisafisha kundi hilo la kigaidi na jinai ya kuchinja kichwa cha mtoto mdogo ni jitihada zilizofeli kwa sababu kundi hilo halishikamani na misingi yoyote ya kimaadili wala kidini
Jumanne iliyopita kundi la kigaidi lilalojiita Nureddin al-Zenki lilitenda ukatili wa kutisha wa kumchinja mtoto Abdullah Issas wa Kipalestina aliyekuwa akiishi katika kambi ya wakimbizi ya Handarat huko Halab kwa tuhuma kwamba alikuwa mwanachama wa al-Quds Brigades.
Hata hivyo imebainika kuwa, mtoto huyo wa Kipalestina aliyekuwa na mri wa miaka 12 hakuwa mwanachama wa kundi lolote na alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Thalassemia (sickle cell).
Kabla ya kumuua, wanachama wa kundi hilo la kigaidi wanaoungwa mkono na nchi kama Marekani, Saudi Arabia na Uturuki walimtaka mtoto huyo aeleze matarajio yake ya mwisho akaomba wamuue kwa kumpiga risasi badala ya kumchinja. Wapiganaji wa kundi la Nureddin al-Zenki walikataa ombi hilo na kuamua kumchinja kama mbuzi.
Post a Comment
Post a Comment