Waziri Mkuu wa Ufaransa ameonya kuhusu hatari ya kuhujumiwa Waislamu wanaoishi nchini humo.

Manuel Valls aliyasema hayo  Jumatano katika Bunge la Senate mjini Paris alipowasilisha muswada wa sheria ya 'kuongeza hali ya hatari Ufaransa.'

Valls ametahadharisha kuhusu Waislamu kushambuliwa kufuatia hujuma za kigaidi nchini humo na kusema uhasama kama huo utapelekea Ufaransa kutumbukia katika vita virefu na vigumu.
Waziri Mkuu wa Ufaransa ameashiria hujuma ya hivi karibuni ya kigaidi nchini humo na kusema, hakuna shaka kuwa Ufaransa itashuhudia hujuma kama hizo siku za usoni.

Waziri Mkuu wa Ufaransa alisisitiza kuwa kuwa: "Watu wa nchi hii wanapaswa kudumisha umoja wao katika kukabiliana na ugaidi kwani ugaidi unalenga kuibua wahka na hofu katika jamii na kupeleka kuwepo uhasama baina ya makundi mawili ya kijamii."

Ameongeza kuwa raia wote wa Ufaransa, wakiwemo Waislamu wanapaswa kuunga mkono utamaduni wa Kiislamu.

Manuel Valls ametoa kauli hiyo wakati ambao kumeibuka wimbi jipya la chuki dhidi ya Uislamu Ufaransa na kote Ulaya kufuatia hujuma ya mjini Nice.

Pamoja na kuwa kwa miaka mingi Waislamu Ufaransa wamekuwa wakiishi na raia wengine wa Ulaya kwa amani lakini katika kipindi cha miaka michache iliyopita, kutokana na kuibuka makundi ya magaidi hasa kundi la magaidi wakufurishaji wa ISIS au Daesh, Waislamu wamekuwa chini ya mashinikizo makubwa sana.

Kwa mujibu wa wataalamu, wanasiasa wengi wa nchi za Ulaya wanatumia vibaya suala hilo na kuwafungamanisha magaidi na Waislamu na Uislamu.

Hali ya mgawanyiko nchini Ufaransa ni mbaya kiasi kwamba Rais Francois Hollande naye pia, sambamba na kutoa salamu zake za rambi rambi kufuatia ugaidi wa Nice, amewataka Wafaransa wote wadumishe umoja wa kitaifa.
Weledi wa mambo wanasema kwa kuzingatia kuwa kuna idadi kubwa ya Waislamu wanaoishi Ulaya ambao ni raia wa nchi hizo, kuwa na dhana mbaya kuwahusu ni kosa kubwa na kuwahusisha na ugaidi kutafuruga umoja, jambo ambalo litahatarisha utengamano na kuibua mifarakano sambamba na kueneza ugaidi chini humo.

Pamoja na hayo, wanaoeneza chuki dhidi ya Uislamu wamezidisha mashinikizo dhidi ya Waislamu wa Ufaransa na nchi zingine za Ulaya.
Hii ni katika hali ambayo Waislamu ndio waathirika wakubwa zaidi wa hujuma za kigaidi duniani.
Katika nchi nyingi duniani kama vile Syria, Iraq, Libya, Nigeria, Afghanistan na Somalia Waislamu wamekuwa ndio waathirika wakuu wa hujuma za magaidi wakufurishaji. Hii ni katika hali ambayo nchi za Magharibi ndizo zilizoanzisha makundi hayo ya kigiaidi kama vile ISIS na Al Qaeda kufikia malengo yao ya kibeberu katika nchi za Kiislamu.
Ugaidi hauna dini, utaifa wala rangi, na hivyo nchi zote duniani zinapaswa kushirikana kwa ajili ya kukabiliana na uovu huu ili amani ya kudumu ipatikane duniani.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.