Shirika la majisafi na majitaka jijini Dar es salaam DAWASCO
linaendelea na zoezi la kurekebisha mabomba yote yaliyokuwa yakivujisha
maji katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.
kaimu mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa shirika hilo
Injinia Aron Joseph amesema hatua hiyo ya Dawasco ilalenga kukausha
maeneo yenye madimbwi ya maji yanayotokana na kupasuka kwa mabomba ya
maji na kuokoa upotevu wa maji.
Injinia Aron Joseph amesema, zoezi hilo la kurekebisha na kubadilisha
mabomba yaliyochakaa katika maeneo 10 ya mikocheni, Masaki na
Mwananyamala ili kuokoa maji yanayovuja kabla ya kuwafikia wateja.
Naye mkuu wa Mkoa wa Kinondoni wa Dawasco Bi Judith Hope
Singinika amewataka wakazi wa Kionondoni ambao awajaunganishiwa maji
kufika katika ofisi za DAWASCO ili kuunganishiwa maji kwa bei nafuu.
Post a Comment
Post a Comment