Usiku wa juzi na jana huko nchini Uingereza kulitimuka vumbi na watu kushikana mashat mara baada ya kuchezeka michezo ya kombe la ligi ambayo kwa sasa inaitwa Carabao Cup.
Juzi usiku Man utd alimbamiza Swansea mabao 2-0 wakati Bristol city akamgaragaza Crystal palace magoli 4-1, AFC Bournemouth ikampiga Middlesbrough 3-1 wakati Leicester iksmfunga Leeds utd 3-1, Arsenal akamkanda Norwich 2-1 wakati huohuo Manchester city ikashinda kwa ushindi wa matuta dhidi ya Wolves mara baada ya mpira kuisha 0-0 na kutoka kimasomaso kwa matuta waliposhinda 4-1.
Lakini usiku wa jana, Chelsea ikamgharagaza Everton iliyo katika wakati mgumu jumla ya magoli 2-1 na West Ham wakawashangaza wengi kwa kushinda 3-2 mara baada ya kupata ushindi huo wakitokea nyuma mara baada ya kipindi cha kwanza kubamizwa 2-0.
Baada ya michuano hiyo kutimua vumbi na kushuhudia klabu za ligi kuu nchini humo zikitakata na kufanya vizuri, huku katika kufuzu ni timu moja tu ambayo haijatokea ligi kuu ambayo ni Bristol City.
Sasa robo fainali ya kombe hilo imepangwa jioni ya leo. ambapo Chelsea iliyofuzu mbele ya Everton itamenyana na AFC Bournemouth huku Arsenal itamenyana na West Ham united wakati Leicester city itashuka dhidi ya Manchester city wakati Man utd itamenyana na Bristol city.
Post a Comment
Post a Comment