Hii itakuwa wiki nzuri na yenye mvuto katika nchi ya Cameroon baada ya timu yao ya taifa ya mpira wa miguu kunyakua ubingwa WA AFCON 2017 baada ya kuwabamiza watoto wa Farao wa Misri kwa mabao 2-1.
Timu hiyo ya Cameroon ambayo toka mwanzo wa mashindano haikupewa nafasi na watu wengi ukizingatia baadhi ya nyota wao waligoma kwenda kujiunga na timu hiyo ilianza kwa kufungwa na Mafarao hao katika dakika ya 15 kupitia kwa nyota wa Misri anayeichezea Arsenal, Elneny na mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Misri 1-0 Cameroon.
Kipindi cha pili kilirudi huku Cameroon wakionekana kujiamini sana na ndipo katika dakika ya 59 mchezaji wa Cameroon, N'koulou akasawazisha kwa goli murua.
Na mpira uliendelea na ndipo katika dakika ya 88, Cameroon wakaongeza goli ambalo ndilo lililoipatia ubingwa timu hiyo ambayo si wengi waliipa nafasi ya kutwaa kombe hilo. Na hii ni mara ya kwanza Cameroon kubeba kombe hilo toka mwaka 2002 na huku Misri hii ndio mara ya kwanza kufika katika fainali baada ya kushindwa kushiriki kwa miaka 3 mfululizo kutokana na matatizo ya kisiasa nchini mwao.
Kwa hiyo bingwa wa mashindano hayo ni Cameroon na huku Misri akiwa mshindi wa pili lakini pia Burkina Faso amekuwa mshindi wa tatu.
Post a Comment
Post a Comment