Kocha msaidizi wa Bayern Munich, Paul Clement na kocha wa zamani wa Birmingham City, Gary Rowett wapo kwenye mchuano ambapo mmoja wao anategemewa kuwa kocha mpya wa Swansea City.
Mwanzoni mchezaji wa zamani na aliyewai kuwa kocha msaidizi wa Manchester united, Ryan Giggs ndiye aliyetegemewa kurithi nafasi hiyo ya kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kutokea Wales ambapo alikuwa ndiyo chaguo namba moja kwa timu hiyo baada ya msimu kutokuwa na matokeo mazuri.
Kocha wa Wales ambapo ndipo makazi ya timu hiyo yalipo, Chris Coleman naye pia alipewa nafasi kubwa kuifundisha timu hiyo lakini BBC Sport ikagundua hakuna tena kinachoweza kuendelea baina yao.
Clement alifanyiwa mahojiano katika kuwania kazi hiyo kabla ya Francesco Guidolin kupata kibarua hicho ambae kwa sasa ametupiwa virago.
Alan Curtis, ambaye amekuwa kocha wa muda baada ya kocha mkuu kutimuliwa, anaamini kocha anayekuja anapaswa awe ni Mwingereza na anayelijua soka la kiingereza."Itakuwa sahihi kama kocha atakayekuja atakuwa mwingereza na anayeijua kwa usahihi ligi kuu ya Uingereza," Curtis alisema
Post a Comment
Post a Comment