Mpaka sasa msimamo unaonyesha Chelsea atamaliza mgunguko huu wa kwanza akiwa kileleni. Kwa kuwa Chelsea wanaongoza msimamo kwa tofauti ya point 6 ambapo yeye ana point 46 huku anaemfata ambaye ni Liverpool akiwa na point 40.

Huku nafasi ya 2, 3, 4 zikiwa bado hazijaeleweka mpaka sasa.

Lakini radha ya mechi hizi za kukamilisha mzunguko wa kwanza inakuja katika kugombania nafasi ya pili. Hapa kuna timu tatu ambazo zinagombania nafasi hiyo Liverpool, Manchester city na Arsenal.

Liverpool ambaye ana point 40 anacheza na Manchester city mwenye point 39 ambapo kama Liverpool inayonolewa na Klopp ikishinda mechi hiyo watajihajikishia nafasi ya pili wakati kama wakitoa droo na Arsenal akishinda basi Arsenal waliochini ya kocha mfaransa, Arsene Wenger watapanda mpaka nafasi ya pili wakiwa na point 42 kama wakishinda. Lakini pia kama Manchester city ambao wanamkosa kwa mara nyengine tena kiungo wao mahiri, Iikay Gundogan kama wakishinda dhidi ya Liverpool usiku wa leo kwenye mishale ya saa 20:30 basi wataingia mwaka mpya wakiwa nafasi ya 2

Kwa upande wa Tottenham itakuwa ngumu kushushwa kutoka kwenye nafasi ya 5 ambapo aliye chini yake ambaye ni Manchester united amezidiwa point 3 na tofauti ya magoli 11 kwa maana hiyo Manchester united ili kumshusha Tottenham itawalizimu washinde mechi yao dhidi ya Middlesbrought kwa jumla ya mabao 12 wakati huo Tottenham afungwe.

Huu ndo utamu wa Ligi kuu Uingereza ulipo.








Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.