Mkurugenzi wa FBI James Comey alisema kuwa baada ya kupitia mawasiliano yote kutoka kwa mgombea wa chama cha Democratic wakati alipokuwa Waziri wa Mamshauriano ya Kigeni, Idara zake zimegundua kuwa hana hatia na hawatamfungulia mashitaka.
Mwezi Julai, baada ya mwaka mmoja wa uchunguzi, James Comey alitangaza katika taarifa yake rasmi kwamba FBI inaamuru kutomfungulia mashitaka Hillary Clinton.
Lakini tangazo la kuanzishwa kwa uchunguzi wa ziada kuhusu barua pepe za Hillary Clinton siku kumi zlizopita, lilizua wimbi hali ya mtafaruku nchini Marekani. Wakati huo Bi. Clinton alionekana akipoteza idadi kubwa ya wapiga kura dhidi ya mshindani wake Donald Trump wa chama cha Republican. Tangu wakati huo utafiti unaonyesha kuwa wagombea hawa walikua wakikaribiana, licha ya Bi. Clinton kuongoza katika utafiti huo.
"Tunafurahi kuona suala hili limeatuliwa," alisema Jumapili usiku mkurugenzi wa mawasiliano wa Hillary Clinton, Jennifer Palmieri. Wakati ambapo pande zote mbili zilikua zikiendesha kapmeni katika maeneo mbalimbali kwa minajili ya kutafuta wapiga kura
Post a Comment
Post a Comment