Leo katika wasifu tunamzungumzia mgombea urais wa Marekani ambapo uchaguzi mkuu unategemewa kufanyika mwezi Novemba, Donald Trump.
Donald Trump ambaye ni mgombea wa urais kupitia chama cha Republican alizaliwa 14, June.1946 ambapo kwa sasa ana miaka 70 katika kitongoji cha Queens kilichopo New York City. Ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watano ambapo baba yake anaitwa Fred Trump na mama yake anaitwa Mary Anne MacLeod. Kaka yake Donald Trump alifariki mwaka 1981 kutokana na ulevi na uvutaji sigara kupindukia ambapo mpaka hii leo Donald Trump hataki kabisa kutumia vitu hivyo.
Donald Trump ni baba wa watoto watano ambapo watoto wake watatu ambao ni Donald Trump Jr, Ivanka Trump na Eric Trump alizaa na Ivana Zelnickova na mtoto wake mmoja aitwaye Tiffany Trump aliyezaa na Maples na mtoto wake mwengine ambaye ni wa tano anaitwa Barron Trump aliyezaa na Knauss.
Donald Trump mwenyewe ni mfanyabiashara akiwa anamiliki hotel kadhaa na baadhi ya kampuni ambapo pia ni mwenyekiti wa Donald Trump Organization. Lakini pia anamiliki vitega uchumi kadhaa vinavyomfanya kuwa na utajiri wa US$4.5 Billion.
Lakini pia Trump ana bachelor's degree ya uchumi ambapo baada ya kutunukiwa shahada hiyo alipata ajira katika organization ya baba yake lakini baada ya muda fulani akairithi organization hiyo na kuiendeleza na ndipo akaiita Donald Trump Organization.
Lakini pia bila kusahau jamaa huyu pia alikuwa mwanajeshi wa jeshi la Marekani.
Post a Comment
Post a Comment