Kuna baadhi ya matukio kadhaa yanayoendelea kutokea nchini Tanzania. Wabunge na wasanii kucheza mechi kucheza soka ili kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, asante kwa soka safi ambalo tumeliona weekend iyo iliyoisha.
Lakini wakati hayo yakiendelea kutokea kuna movie moja inaendelea pale katika chama kimojawapo cha upinzani nchini hapa. Chama cha wananchi, CUF kuna mzozo unaendelea ambao haijulikani ni lini zengwe hilo litaisha.
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye uchaguzi uliopita aliamua kujiunga na muungano wa vyama pinzani ili kumsimamisha mgombe mmoja atakayewakilisha upinzani kilichoitwa UKAWA.
Baada ya uchaguzi kupita na vuguvugu zote zilizotokea na uchaguzi kupita mwisho wa siku chama tawala cha CCM kikaendelea kushika madaraka.
Baada ya muda mfupi kupita mwenyekiti huyo wa CUF akaita waandishi wa habari na kuelezwa majuto yake ya kuwa chini ya umoja huo wa vyama vya upinzani.
Baada ya movie hiyo kuendelea japo iliwaacha watu na maswali mengi bila majibu, mchana wa leo katika kikao cha chama hicho cha CUF, mwenyekiti huyo amefukuzwa kutokana na baadhi ya wanachama kusema hawamtambui kwa kuwa alishajiengua katika nafasi hiyo ya uenyekiti. Ikumbukwe pia Profesa huyo mwenye utaalamu na mambo ya uchumi amekiongoza chama hicho kwa vipindi vingi vya uchaguzi mkuu nchini Tanzania.
Post a Comment
Post a Comment