Katika jimbo la Gao, kaskazini mwa Mali, serikali imepiga marufuku maandamano ya aina yeyote licha ya kuwa yamefanyika Jumanne hii asubuhi
maandamano haya yametokea baada ya Vijana kuitikia wito wa mashirika kadhaa ya kiraia wa kuandamana dhidi ya kuanza kazi kwa viongozi wa mpito waliyowekwa kulingana na makubaliano ya Algiers.
Mkutano huo uligubikwa na machafuko ulifanyika Jumanne mchana, huku milio ya risasi ikiripotiwa  kusikika katika mitaa mbalimbali ya mji.
kwa mujibu wa wakazi wanasema Maeneo manne kati ya saba ya mji wa Gao yalikumbwa na vurugu hizo.
Vijana kadhaa wameingia mitaani Jumanne asubuhi licha ya kupigwa marufuku na manispaa ya jiji ambayo ilibaini kuwepo kwa hali ya hatari katika mitaa hiyo.
Vikosi vya usalama vilitumwa ili kutoa ulinzi katika mitaa ya mji huo lakini  Vijana walirusha mawe,na polisi wakajibu kwa kutumia mabomu ya machozi.
Kwa mujibu wa mashahidi, askari polisi walianza kurusha risasi za moto hewani ili kuzuia vurugu kubwa iliyokuweko.
Idara ya dharura katika hospitali ya mjini Gao imethibitisha vifo vya watu wawili na wengine 17 kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wawili wakiwa katika hali mbaya.
Kwa mujibu wa mkuu wa Idara hiyo, vijana waliojeruhiwa wamekua wakiendelea kuingizwa kwa wingi hospitalini, na idadi inatarajiwa kuongezeka.
Hali bado ni tete, na mkuu wa jimbo la Gao ametoa wito kwa raia kuwa watulivu.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.