Magoli mawili ya kiungo wa atletico Madrid Antonnie Griezman yalitosha kabisa kuisambaratisha ujerumani katika nusu Fainal iliyopigwa katika dimba La Marseille huko ufaransa.
Magoli hayo yaliyofungwa kila kipindi yameiwezesha ufaransa kukata tiketi ya kucheza Fainali itakayopigwa siku ya jumapili dhidi ya ureno ambayo hapo jana iliitandika wales mabao mawili nunge.
Mechi hiyo iliyokuwa imejaa ufundi wa kila aina ilianza kwa kasi sana ambapo ndani ya dakika za mwanzoni kabisa ufaransa walikosa goli LA wazi huku griezman akipiga shuti ambalo halikuwa na madhara kwa Neure.
Kadri ya dakika zilivyozid kwenda,ujeruman walianza kuingia mchezoni na kuanza kumiliki mpira huku wakisababisha madhara na kosa kosa nyingi katika lango la ufaransa.
Mechi ilidumu ivo mpaka pale Bastian shweinzteiger aliponawa mpira katika eneo la hatari na kuwapa penati ufaransa ambayo griezman alimuuza neure.
kipindi cha pili kilianza kwa ufaransa kutawala mpira mpaka pale walipokuja kupata bao lapili.
FAINALI : UFARANSA VS URENO
Nani kimfunga paka kengele jumapili?
Post a Comment
Post a Comment