Klabu ya Yanga ya Dar es salaam Tanzania leo imepoteza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika kwa kufungwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa dimba la Taifa Dar es salaam.
Katika mchezo huo ambao mashabiki wameingia bure na kuutapisha uwanja, Yanga imeonesha kandanda safi katika kipindi cha kwanza, kabla ya TP Mazembe kutoka DRC kubadilika katika kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao hilo lililofungwa dakika ya 74 na kiungo Merveille Bope baada ya mabeki wa Yanga kujichanganya, kutokana na mpira wa adhabu ndogo.
TP Mazembe walipata mpira huo wa adhabu hiyo baada ya mshambuliaji wao mtanzania Thomas Ulimwengu kuangushwa nje kidogo ya ya 18 na beki wa Yanga Kelvin Yondan, ambaye pia aliadhibiwa kwa kupewa kadi ya njano.
Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga kupoteza ukitanguliwa na ule uliochezwa nchini Algeria Juni 19 na kufungwa bao 1-0 na MO Bejaia.
Kwa matokeo haya, hadi sasa TP Mazembe inasalia kileleni kwa kuwa na pointi 6, huku Yanga ikiwa haina point hata moja, katika kundi A.
Mchezo mwingine katika kundi hilo utakaowakutanisha Medeama ya Ghana dhidi ya MO Bejaia ya Algeria unapigwa kesho saa 12 jioni nchini Ghana.

Baada ya mchezo huu, Yanga inajipanga kuwaalika Medeama ya Ghana, mchezo utakaopigwa Julai 15 katika dimba la Taifa Dar es salaam.
Post a Comment
Wamefungwa ENGLAND sembuse YANGA!!!!
Wamefungwa ARGENTINA sembuse YANGA!!!
haha!! haha WAKIMATAIFA!!!!!! watoto wajangwani noma sana.Nashaangaa sana Watanzania waliokua wakishabikai Wageni.
kufa kufa tuu
Post a Comment