Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza asilimia 60 ya mapato yanayopatikana katika mifuko ya afya kutumika kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.
Waziri MWALIMU amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu mkoa wa TABORA, MUNDE TAMBWE aliyetaka kufahamu mpango wa serikali katika kuboresha huduma za afya kwenye mikoa ya Tabora, Katavi na Simiyu.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI, SELEMANI JAFFO amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi Bilioni 131 ikiwa ni fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule, chakula, mitihani na fidia ya ada.
Amesema fedha hizo zitapelekwa moja kwa moja katika shule kwa wastani wa zaidi ya shilingi bilioni 18 kwa mwezi.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi MWIGULU NCHEMBA amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watendaji kukamata bidhaa za wafanyabiashara ikiwemo samaki na kuzitumia kwa manufaa yao.

Waziri NCHEMBA ameagiza wote watakaobainika kuhusika kukamatwa na kuchukuliwa hatua kama wezi wengine ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao kwa kuzingatia taratibu
Post a Comment
Post a Comment