Serikali ya Somalia inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa kuwaachilia huru waandishi wawili wa habari waliokamatwa siku ya Ijumaa.
Wawili hao walitiwa mbaroni baada ya kituo chao cha habari cha Universal TV kupeperusha hewani mjadala wenye utata.Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay, amesema kwamba kuzuiliwa kwa mtangazaji Awil Dahir Salad na msimamizi Abdullahi Hersi, ni tishio kwa uhuru wa vyombo vya habari.
Post a Comment
Post a Comment