Vijana wa Lowasa zaidi ya 4000 watelekezwa Dodoma
Wadau, taarifa nilizopata hivi punde kutoka Dodoma zinasema kuwa vijana zaidi ya 4000 ambao walichukuliwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kuongeza hamasa kwa Lowasa wengi wao wakitoka Arusha na Manyara wametelekezwa. Taarifa nilizopata kutoka kwa mdau wangu ambaye ni miongoni mwa wahanga hao amesema kuwa tangu walipopata taarifa kuwa Lowasa hayumo kwenye tano bora, hali ya maisha yao yamekuwa magumu. Kwamba, wakati wanajiandaa kwenda Dodoma, waliahidiwa kuwa watagharamiwa chakula, usafiri wa kwenda na kurudi Dodoma, malazi na posho. Hata hivyo, mtoa taarifa huyo amesema kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Lowasa kaenguliwa, hawapati huduma hizo kama walivyoahidiwa.
Taarifa zinasema kuwa baadhi ya vijana wamerejesha vyumba walivyochukuliwa kwenye nyumba za kulala wageni na badala yake wanashinda barabarani na kukesha kwenye bar kwa vile hawana pa kulala. Aidha, mtoa taarifa huyo anasema kuwa baadhi ya vijana hao wanalala mzungu wa nne kwa uwiano wa vijana wanne kitanda kimoja.
Kutokana na hali hiyo, mtoa taarifa huyo anasema kuwa vijana hao wanapanga kumuona Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM awasaidie japo wafanikiwe kurejea kwao. Kwa mapendekezo yao, wanaomba kuwa zile fedha zilizokamatwa ambazo inasemekena kuwa ni za Team Lowasa wapewe sehemu ya fedha hizo ili wapate nauli ya kurejea kwao. Pia wanasema kuwa watakapomuona Rais Kikwete ambaye ndiye mwenyekiti wa CCM, watamuomba awaamuru viongozi wao watoe yale Mabasi ya Safari ha Matumaini ambayo ndiyo walitumia kwenda Dodoma yawasafirishe kurejea kwao.
Vijana hao ambao wengi wao wapo maeneo ya Nyerere Square wanajuta kutumika na wanasiasa na wanakumbuka maneno ya Mwenyekiti wa CCM, Kikwete alipowatahadhalisha kuwa wasitumike na wanasiasa. Wanakumbuka pia yale masimulizi aliyotoa Kikwete kuwa kuna mgombea aliwatelekeza wapiga kura wake mara baada ya kukosa ushindi. Wanasema kuwa ndivyo inavyowatokea. Hata hivyo, wanahisi kuwa huenda viongozi wao ndio waliowadhulumu na kwamba kabla hawajamuona Rais, wana mpango wa kumuona Hussein Bashe, ama Emmanuel Nchimbi, ama Peter Serukamba ili wapate ufafanuzi wa hoja zao.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.