uKikosi cha timu ya taifa ya Brazil kimeigaragaza timu ya taifa ya Japan katika mchezo uliochezeka jioni ya leo.
Mabao 3-1 ndio yaliyoipa ushindi Brazil iliyojumuisha mastaa wake kama kawaida.
Alikuwa ni Neymar, mchezaji ghali duniani aliyeanza kufungua karamu ya magoli katika mchezo huo mara baada ya kuifungia Brazil goli kwa njia ya penati.
Akafata Marcelo anayeichezea klabu ya Real Madrid ambaye yeye alifunga kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Japan, Kawashima na kufanya ubao kusomeka Brazil 2-0 Japan.
Dakika ya 35 yule namba tisa wa Manchester city, Gabriel Jesus akamaliza karamu ya magoli kwa upande wa Brazil na matokeo kuwa 3-0, Brazil wakiwa mbele huku Neymar akikosa mkwaju mwengine wa penati katika kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili dakika ya 65, Makino wa Japan akaisawazishia Japan bao la kufutia machozi na kufanya mchezo kuisha Brazil wakitoka kimasomaso kwa ushindi wa mabao 3-1.
Wakati hayo yakitokea kwa Brazil, majirani zao wanaotoka bara moja la Amerika ya Kusini, Colombia imepokea kichapo katika mchezo mwengine wa kirafiki ambapo imefungwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Jamhuri ya Korea. Mabao yote mawili ya Korea yakifungwa na nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Heung-Min Son wakati huku bao pekee la Colombia likifungwa na Christian Zapata.
Post a Comment
Post a Comment