Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka Marekani iimarishe silaha zake za nyuklia, hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza kuzungumzia silaha za nyuklia tangu aingie madarakani.
Bw Trump amesema inaweza kuwa vyema sana iwapo hakungekuwa na taifa lolote lililo na silaha za nyuklia duniani.
Lakini amesema iwapo hilo haliwezekano, basi Marekani itahakikisha kwamba inakuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa silaha za nyuklia.

Ameambia shirika la habari la Reuters kwamba Marekani "imeachwa nyuma sana katika uwezo wake wa silaha za nyuklia".

Wakosoaji hata hivyo wanasema Marekani na Urusi tayari zina silaha za kutosha za nyuklia kuzuia taifa lolote kushambulia jingine kwa nyuklia.

Marekani ina silaha 6,800 za nyuklia na Urusi 7,000, kwa mujibu wa chama cha udhibiti wa silaha cha Marekani.

Akiongea na Reuters, Bw Trump amesema: "Mimi ndiye mtu wa kwanza ambaye angependa kuona kwamba hakuna mtu aliye na silaha za nyuklia, lakini hatutakubali kuachwa nyuma na taifa lolote lile, hata kama ni taifa rafiki, hatutaachwa nyuma katika uwezo wa nyuklia."
"Linaweza kuwa jambo zuri, ndoto nzuri ambapo hakuna taifa lingekuwa na silaha za nyuklia, lakini iwapo mataifa yatakuwa na silaha za nyuklia, tutakuwa miongoni mwa wanaoongoza."

Matamshi yake hayo yanakariri ujumbe alioandika kwenye Twitter wiki chache zilizopita baada yake kushinda uchaguzi wa urais, ambapo aliahidi kuimarisha uwezo wa nyuklia wa Marekani.
Mkataba wa kupunguza silaha za nyuklia kati ya Marekani na Urusi, ambao unaitwa New Start (Mwanzo Mpya) unazitaka nchi hizo mbili, kufikia 5 Februari mwaka ujao, kupunguza silaha zao kwa kiasi sawa kwa miaka 10.
Chama cha udhibiti wa silaha cha Marekani, ambalo ni shirika huru lisiloegemea upande wowote, limekosoa tamko la Trump.

"Matamshi ya Trump, kwa mara nyingine, yanaonesha kwamba hana ufahamu mzuri kuhusu silaha za nyuklia na hafahamu hatari zinazotokana na silaha hizo," shirika hilo limesema kupitia taarifa.
"Historia ya Vita Baridi inatuonesha kwamba hakuna anayeibuka na ushindi katika mbio za kulimbikiza silaha na kuimarisha silaha za nyuklia.

source
bbc.com/swahili

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.