Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) imepunugzia adhabu ya kusimamishwa kwa Maria Sharapova kutoka miaka miwili hadi miezi 15.
Mchezaji huyo wa Urusi alisimamishwa kwa muda wa miaka miwili na Shirikisho la Kimataifa Juni 8, baada ya kukiri kwamba alikuwa akitumia dawa ya Meldonium tangu mwezi Januari. Dawa hii ni miongoni mwa dawa zilizopigwa marufuku na Shirikisho hilli.
Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo imechukua uamuzi kwamba bingwa wa zamani wa dunia alikuwa na hatia ya 'ukiukaji wa sheria za kupambana na madawa ya kusisimua mwili,' lakini 'hajafanya kosa kubwa'.
"Kama tarehe ya kusimamishwa ilianza kutekelezwa Januari 26, 2016 , tarehe ambayo alipimwa na kugundulika kuwa anatumia dawa hiyo katika michuano ya Open Australia, ataweza kuanza mashindano Aprili 26, 2017, mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa michuano ya kimataifa ya nchini Ufaransa, katika mji wa Roland-Garros.
Post a Comment
Post a Comment