Batshuayi:Mshambuliaji wa Ubelgiji,Michy Batshuayi,22,amefuzu vipimo vya afya na muda wowote atasaini kandarasi ya miaka mitano ya kuichezea Chelsea kwa ada ya £33.2.Batshuayi,22,amefanyiwa vipimo hivyo leo mchana huko Bordeaux baada ya klabu yake ya Marseille kumkutanisha na daktari wa Chelsea aliyesafiri mpaka katika mji huo kukamilisha zoezi hilo.Msimu uliopita Batshuayi aliifungia Marseille mabao 23.(L’Equipe)
Takuma:Arsenal imeripotiwa kutuma ofa ya zaidi ya £2m kwenda Sanfrecce Hiroshima ya Japan kwa ajili ya kutaka kumsajili mshambuliaji kinda wa klabu hiyo,Takuma Asano,21.(Sanyo News)
Messi:Mashabiki zaidi ya 100,000 wa Argentina wamethibita kuwa watashiriki katika maandamano ya kumshawishi staa wa nchi hiyo Lionel Messi ili arejee kwa mara nyingine kuichezea timu yao ya taifa.(SPA)
Wenger:Meneja wa Arsenal,Arsene Wenger ameendelea kuwaweka roho juu mashabiki wa klabu hiyo baada ya kushindwa kukiri ama kukana habari zinazodai kuwa kocha huyo raia wa Ufaransa anataka kumsajili mshambuliaji wa Lyon,Alexandre Lacazette,mwenye thamani ya £45m.Lacazette,25,ameifungia Lyon mabao 54 katika michezo 83.
Ake:Mlinzi wa kushoto wa Chelsea,Nathan Ake, amejiunga na Bournemouth kwa mkopo wa msimu mmoja.Ake,21,ambaye pia msimu uliopita aliichezea Watford kwa mkopo amelazimika kusaka klabu nyingine kwa msimu mmoja zaidi hii ni baada ya Chelsea kushindwa kumhakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi chake cha kwanza.
Nani:Rais wa Fenerbahce,Aziz Yildirim ametangaza kuwa winga wa klabu hiyo Mreno Luis Nani,28,ataihama klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Valencia mara baada ya kuisha kwa michuano ya Euro. (AMK Sport)
Hulk:Shanghai SIPG imevunja rekodi ya usajili katika historia ya soka la China na Asia yote baada ya leo kumsajili staa wa Brazil,Hulk kwa kitita cha €50m toka Zenit St Petersburg.(O'jogo)
Byram:Arsenal imeripotiwa kuwa itamsajili mlinzi wa kulia wa West Ham,Sam Byram,ikiwa mlinzi wake, Hector Bellerin,ataamua kujiunga na Barcelona katika kipindi hiki cha usajili.Byram,22,alijiunga na Westham mwezi Januari akitokea Leeds United na tangu wakati huo amefanikiwa kucheza michezo minne pekee ya Ligi Kuu England.
Gomez:Baada ya kuwakosa Michy Batshuayi na Alexander Lacazette,Westham imeripotiwa kuanza mazindo ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na
Besiktas,Mario Gomez,28.(Mirror)
Mikel:Kiungo wa Chelsea,John Obi Mikel ameripotiwa kuwa atatimka klabuni hapo ikiwa kocha mpya wa klabu hiyo,Antonio Conte,atashindwa kumhakikishia nafasi ya kucheza mara kwa mara.
Post a Comment
Post a Comment