Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa haitasherehekea uhuru wake mwaka huu kutokana na uhaba wa fedha.
Waziri wa habari Michael Makuel Lueth amesema kuwa maadhimisho ya tano ya uhuru wa taifa hilo yatafanyika kwa ukimya.Serikali pia inasema haitanunua magari ya kifahari kwa mawaziri wapya.
Tangu taifa hilo lijinyakulie uhuru wake kutoka kwa Sudan,limekubwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na mgogoro wa kiuchumi.
Sarafu yake imashuka na wafanyikazi wa serikali hawawezi kutosheka na mishahara yao ambayo hulipwa kuchelewa.
Post a Comment
Post a Comment