Timu ya Iceland imeoiondoa England kwa mabao 2-1 katika michuano ya mpira ya Euro 2016 inayoendelea nchini Ufaransa.
Kipigo hiko kimepelekea kujiuzulu kwa kocha wa timu hiyo Roy Hodgson,ambaye ameelezea hayo mara tu bada ya kumalizika kwa mchezo huo katika mkutano na waandishi wa habari akiwa ameiongoza kwa miaka minne.
Iceland kwa sasa itakutana na mwenyeji wa michuano hiyo Ufaransa mjini Paris Jumapili Julai 3.Katika mchezo mwingine bingwa mtetezi Hispania ameondolewa kwa kichapo cha 2-0 ilipokipiga dhidi ya Italia.
Post a Comment
Post a Comment