Rapper Nikki wa Pili amesema kwake yeye Cristiano Ronaldo ni zaidi ya Lionel Messi katika ubora wa soka.
Akizungumza na mtangazaji wa kipindi cha Michezo Leo cha Metro FM ya Mwanza Moses William, Nick amesema sababu kubwa ya kumtaja Ronaldo kuwa ni zaidi ya Messi ni kutokana na uwezo aliouonesha katika michuano ya UEFA na EURO na kuisaidia timu yake ya Real Madrid na timu yake ya taifa ya Ureno kutangazwa mabingwa wa Ulaya 2016.
Kutokana na Argentina kupoteza mchezo wake wa fainali na Ureno kushinda mchezo wa Fainali dhidi ya ufaransa Nick alisema,” Nampa nafasi kubwa Cristiano Ronaldo kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa DUNIA(Ballon d’Or) msimu huu kutokana na kufanya kwake vizuri katika michuano ya Ulaya(UEFA) ngazi ya klabu na timu ya taifa(EURO) kwani Ureno ilikuwa haipewi nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa lakini chini ya uongozi shupavu wa Ronaldo hilo likawezekana.”
Nick aliongeza kuwa mazingira ambayo yaliiwezesha Ureno kutwaa ubingwa inaweza ikawa ni credit kubwa kwa Ronaldo kutwaa (Ballon d’Or) msimu huu tofauti na mazingira ya timu ya Argentina chini ya Messi iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kutokana na ubora wa kikosi chao lakini walipoteza katika mchezo wao wa fainali dhidi ya Chile.
Hicho ni moja ya vigezo vinavyoangaliwa kwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa DUNIA (Ballon d’Or). Mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa January 9 mwaka 2017 huku majina ya watakaowania yakitajwa Novemba mwaka huu.
by
Bongo 5

Post a Comment
Post a Comment